Nyumbani
Fainali mabingwa mikoa kundi B leo

FAINALI za Ligi ya Mabingwa Mikoa 2023 zinaendelea leo kwa michezo miwili ya kundi B kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi mkoa wa Kilimanjaro.
Wakati wa mchana Mapinduzi ya Mwanza itavaana na Ilula Tigers ya Iringa wakati Malimao ya Katavi itatinga dimbani dhidi ya Nyumbu ya Pwani katika mchezo wa pili.
Katika mechi za kundi A zilizopigwa Aprili 25 Kiluvya ya Dar es Salaam imeichapa Annuary ya Shinyanga mabao 2-1 wakati Tanzania Navy ya Dar es Salaam imepokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka TANESCO ya Kilimanjaro.