Ligi KuuNyumbani

Kagera kuizuia Yanga leo?

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Dar es Salaam huku mechi kivutio ikiwa Yanga kuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Azam Complex.

Kuelekea mchezo huo Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema klabu hiyo imejiandaa vizuri kushinda mechi hiyo.

“Changamoto kubwa tunaweza kusema ni ratiba tuliyonayo, mechi zinakaribiana sana, mfano tuna mechi za kimataifa, mechi za ligi na FA, lakini mbali na hivyo sisi benchi la ufundi tunawaandaa wachezaji wetu vizuri kupata matokeo mazuri kwenye kila mchezo,”amesema Kaze.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 65 baada ya michezo 24 wakati Kagera Sugar ipo nafasi ya 7 ikijikusanyia pointi 32 baada michezo 25.

Nayo Geita Gold itakuwa mgeni wa KMC kwenye uwanja wa Uhuru. Geita Gold inashika nafasi ya 6 ikiwa na pointi 34 baad aya michezo 25 wakati KMC ni ya 14 ikiwa na pointi 26.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button