Africa

Yanga kuifuta Mazembe Machi 30

KLABU ya Yanga itaondoka nchini Machi 30 kwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa ajili ya mchezo wa mwisho Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Aprili 2.

Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe amesema katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kwamba wachezaji wa timu hiyo ambao hawajaitwa timu za taifa watarudi rasmi mazoezini Machi 23 na kisha kambi rasmi ya mazoezi itaanza Machi 27 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.

“Timu tunatarajia itaondoka Dar es Salaam kwenda Lubumbashi, Congo tarehe 30 na shirika la ndege la Air Tanzania na kuna baadhi ya Wachezaji walioitwa kwenye majukumu ya timu za taifa tutajumuika nao pamoja Congo,”amesema Kamwe.

Yanga ambayo tayari imefuzu robo fainali inaongoza kundi D ikiwa na alama 10 sawa na US Monastir lakini ina magoli mengi zaidi ya kufunga huku AS Real Bamako ikiwa nafasi ya tatu kwa alama 5 wakati TP Mazembe ni ya mwisho ikiwa na alama 3.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button