AFCONAfricaAfrika Magharibi

Chris Hughton kocha mpya Ghana

CHAMA cha Soka Ghana(GFA) kimemtambulisha Chris Hughton kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo(Black Stars).

Kocha huyo wa zamani wa Newcastle amesaini mkataba wa miaka miwili hadi Disemba 2024.

Akizungumza baada ya kutambulishwa Hughton amesema yupo tayari na anajivunia kupewa jukumu kukinoa kikosi cha Black Stars.

“Kuwakilisha Ghana na Black Stars kama kocha mkuu ni jambo ambalo ninajivunia sana. Nitafanya kila linalowezekana kuhakikisha timu inafanikiwa,” amesema Hughton.

Mchezo wa kwanza Hughton akiwa na Ghana utakuwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 dhidi ya Angola Machi 23 kwenye uwanja wa Baba Yara, Kumasi na baadaye marudiano mjini Luanda, Angola.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button