
LIGI ya Soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja, KMC ikiwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kagera Sugar inashika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 32 baada ya michezo 24 wakati KMC ni ya 13 ikikusanya alama 23.
Katika michezo mitano ya mwisho ya ligi kati ya timu hizo Kagera Sugar imeshinda mara 3, KMC mara 1 na zimetoka sare mara 1.