Africa
Yanga dimbani leo

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga leo inashuka dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kupambana na AS Real Bamako ukiwa mchezo wa marudiano wa kundi D.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika mjini Bamako, Mali timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1.
Michezo mingine ya Kombe la Shirikisho leo ni kama ifuatavyo:
Kundi A
Marumo Gallants vs USM Alger
Al-Akhdar vs Saint-Eloi Lupopo
Kundi B
Rivers United vs Motema Pembe
Diables Noirs vs ASEC Mimosas
Kundi C
ASKO Kara vs Pyramids
Future vs FAR Rabat
Kundi D
US Monastir vs TP Mazembe