Nyumbani

Amrouche kocha mkuu mpya Taifa Stars

SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limemtangaza Adel Amrouche kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Taarifa ya TFF imesema Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria mwenye umri wa miaka 58 ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika baada ya kufundisha klabu na timu za taifa katika ukanda wa Kusini, Mashariki, Kati na Kaskazini.

Timu alizowahi kuzifundisha ni pamoja na DC Motema Pembe, RC Kouba, USM Alger na MC Agiers.

Timu za Taifa ni Kenya, Equatorial Guinea, Botswana, Libya, Burundi na Yemen.

TFF imesema kocha Adel ana leseni ya Uefa Pro na shahada ya uzamili katika kuwasoma watu na utimamu.

Aidha kwa mujibu wa TFF, katika wakati wote wa mkataba wake kocha Amrouche ambao haikusema ni wa muda gani atalipwa mshahara na serikali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button