
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili Dar es Salaam na Tanga.
Coastal Union inayoshika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi yenye alama 22 baada ya michezo 23 ni mwenyeji wa Tanzania Prisons yenye alama 22 pia kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, KMC iliyopo nafasi ya 12 yenye alama 23 itakuwa mgeni wa Azam inayoshika nafasi ya 3 ikiwa na alama 44.