Africa
Simba dimbani leo Ligi ya Mabingwa Afrika

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba leo inashuka dimbani kuikabili Horoya ya Guinea.
Mchezo huo wa kwanza kwa Simba iliyopo kundi C utapigwa kwenye uwanja wa Jenerali Lansana Conte uliopo mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry.
Michezo mingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayofanyika leo ni kama ifuatavyo:
Kundi A
Pedro Atletico vs JS Kabylie
Kundi B
Mamelodi Sundowns vs Al Hilal Omdurman
Kundi D
Esperance vs Al-Merreikh