Ligi KuuNyumbani

Bruno Gomez mchezaji bora Januari

MCHEZAJI wa klabu ya Singida Big Stars Bruno Gomez amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara msimu wa 2022/23.

Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imesema Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF) imemchagua Gomez baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Januari na kutoa mchango mkubwa kwa Singida ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili na kusaidia timu yake kupata alama sita katika michezo miwili iliyocheza.

Gomez amewashinda Ibrahim Abdallah wa Namungo na Henock Mayala wa Polisi Tanzania alioingia nao fainali.

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kamati hiyo imemchagua Kocha Mkuu wa Singida Big Stars Hans Pluijm kuwa kocha bora wa Januari.

Pluijm amewashinda Roberto Oliveira wa Simba na Nasreddine Nabi wa Yanga alioingia nao fainali baada ya kuiongoza Singida Big Stars kushinda michezo miwili iliyocheza mwezi huo na kuendelea kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.

Pia kamati hiyo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Highland Estates Mbarali, Malule Omary kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi Januari kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button