Michezo Mingine

Jack Cambell apata ahuweni baada ya kuangukia shingo

DETROIT: KIKOSI cha Detroit Lions kimetoa taarifa mpya kuhusu hali ya mchezaji wake wa nafasi ya linebacker, Jack Campbell, baada ya kupata jeraha la kutisha la shingo katika mchezo dhidi ya Minnesota Vikings uliochezwa mwishoni mwa wiki.

Campbell alilazimika kutolewa uwanjani kwa machela baada ya kubaki bila kusogea kwa muda, kabla ya kupelekwa katika hospitali moja jijini Detroit kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Taarifa ya hivi karibuni kutoka kwa klabu hiyo imeleta matumaini kuhusu hali yake, ingawa bado anaendelea kupata uangalizi wa kitabibu hospitalini.

Tukio hilo lilitokea katika robo ya nne ya mchezo wa NFL wa wiki ya nane, ambapo Detroit Lions iliibuka na ushindi wa mabao 19-15 dhidi ya Minnesota Vikings. Campbell alipata jeraha hilo wakati mchezo ukiendelea na hali yake ilizua wasiwasi mkubwa kwa wachezaji wenzake, benchi la ufundi pamoja na mashabiki waliokuwa wakifuatilia pambano hilo. Baada ya tukio hilo, wahudumu wa afya waliingia uwanjani kumhudumia kabla ya kuamua kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi wa kina.

Siku ya Jumatatu alasiri, Detroit Lions ilitoa taarifa kuhusu maendeleo ya hali ya mchezaji huyo, ikieleza kuwa bado amelazwa hospitalini jijini Detroit huku akiendelea kupumzika na kupata nafuu. Klabu hiyo ilisema kuwa tathmini za awali za kitabibu zimeonesha dalili zinazotia moyo, ingawa haikutoa maelezo zaidi kuhusu aina halisi ya jeraha au kiwango cha madhara aliyoyapata Campbell.

Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, klabu hiyo ilisema Campbell anaendelea kupumzika na kuimarika katika hospitali ya eneo hilo, huku matokeo ya awali ya uchunguzi yakionesha dalili chanya. Hata hivyo, uongozi wa Detroit Lions ulisisitiza kuwa hautatoa taarifa nyingine za kitabibu kwa sasa kutokana na kuheshimu faragha ya mchezaji huyo na familia yake. Klabu haijabainisha muda ambao Campbell atahitaji kubaki hospitalini wala lini anaweza kurejea katika shughuli za kawaida za timu.

Jeraha hilo limekuwa pigo kwa Detroit Lions kutokana na mchango wa Campbell katika safu yao ya ulinzi. Mchezaji huyo ni sehemu muhimu ya kikosi kinachoshiriki Ligi ya NFL, ambacho kinategemea uwezo wake katika kuzuia mashambulizi ya wapinzani na kusaidia timu kudhibiti mchezo. Hata hivyo, kwa sasa kipaumbele cha klabu ni kuhakikisha anapata matibabu na uangalizi unaohitajika kabla ya kuzungumzia uwezekano wa kurejea uwanjani.

Kwa upande wa mashabiki, taarifa kwamba tathmini za awali zimeonesha matokeo yanayotia moyo imekuwa faraja baada ya tukio lililosababisha hofu kubwa wakati wa mchezo. Hata hivyo, kwa kuwa Campbell bado amelazwa hospitalini na klabu haijafichua maelezo ya kina kuhusu jeraha lake, hali yake inaendelea kufuatiliwa.

Related Articles

Back to top button