Ligi Kuu

Kaze ataja kilichosababisha kufungwa 4-0 na Yanga

KOCHA mkuu wa Kagera Sugar amesema kupoteza mpira kirahisi kulikuwa miongoni mwa changamoto zilizoigharimu timu yake katika mchezo dhidi ya Yanga, uliomalizika kwa kipigo cha mabao 4-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha huyo amesema kurejea mazoezini kutakuwa nafasi ya kushughulikia tatizo hilo ili wachezaji wawe makini zaidi katika michezo ijayo.

Amesema licha ya matokeo hayo, anawashukuru wachezaji wake kwa kujitahidi kucheza vizuri, akieleza kuwa walionesha nia ya kujenga mashambulizi kwa kuanzia nyuma kwenda mbele.

Hata hivyo, amekiri kuwa timu yake ilipoteza nafasi kadhaa za kufunga, akibainisha kuwa Kagera bado ipo katika hatua ya kujijenga ili kufikia kiwango bora zaidi cha ushindani.

Kocha huyo amesema moja ya mambo makubwa aliyojifunza katika mchezo huo ni umuhimu wa kutafakari na kurekebisha makosa, hususan tabia ya kupoteza mpira kirahisi kama walivyofanya walipokutana na Yanga.

Amesisitiza kuwa wataifanyia kazi changamoto hiyo katika mazoezi ili kuimarisha umakini na ushindani wa timu katika michezo inayofuata.

Kagera ilifungwa na Yanaga bao 4-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex Jijini Dar es salaam

Related Articles

Back to top button