
ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amepewa nafasi nyingine ya kuendelea kuiongoza timu hiyo, lakini bado anakabiliwa na presha kubwa huku mustakabali wake ukitegemea matokeo ya mchezo muhimu dhidi ya Chelsea.
Carrick, ambaye amekuwa akikabiliwa na changamoto ya kurejesha makali ya Manchester United, sasa anatarajiwa kukutana na mtihani mzito katika safari ya kuifuata Chelsea. Matokeo ya mchezo huo yanaweza kuwa na athari kubwa katika hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Wakati huo huo, Arsenal inajiandaa kukabiliana na Liverpool katika mchezo unaotarajiwa kuwa kipimo muhimu kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England, katika harakati zao za kulinda taji.
Kwa upande mwingine, Manchester City itakutana na Brighton kwa mara ya pili ndani ya siku nne, katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka.




