EPLKwingineko
Wolves yakubali kumsajili Sarabia

KLABU ya Wolverhampton Wanderers imekubali ada ya pauni milioni 4.4 sawa na shilingi bilioni 12.4 kumsajili winga wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Hispania, Pablo Sarabia.
Sarabia mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kufanya vipimo leo na kusaini dili la miaka miwili na nusu hivyo kuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Wolves katika dirisha dogo.
Alijiunga na PSG mwaka 2019 akitokea Sevilla na tangu wakati huo amefunga mabao 11 katika michezo 35 Ligi Kuu ya Ufaransa(Ligue 1).
Wolves imekamilisha usajili wa Mario Lemina kutoka Nice wakati Desemba 2022 ilimsajili Matheus Cunha kutoka Atletico Madrid kwa dili la awali la mkopo.