Mastaa

Zuchu aanza safari ya kurudisha umbo

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Zuchu, amesema mabadiliko ya uzito wa mwili wake baada ya kujifungua, akieleza kuwa uzito wake uliongezeka kutoka kilo 58 kabla ya ujauzito hadi kilo 82 siku aliyojifungua.

Akizungumzia hali hiyo, Zuchu amesema aliongezeka karibu kilo 30 katika kipindi cha ujauzito, akisisitiza kuwa uzito unaotokana na ujauzito si jambo dogo kama wengi wanavyoweza kufikiria.

“Kilo za uzazi sio kilo za mchezo. Mimi nimeshika mimba nina kilo 58, nimejifungua ile siku natembea pale nina kilo 82, niliongezeka karibu kilo 30,” amesema Zuchu.

Msanii huyo ameongeza kuwa kwa sasa ameanza kupunguza uzito, huku akieleza kuwa anazingatia zaidi vyakula vya majimaji, ikiwemo supu, kupunguza ulaji wa wali.

Hata hivyo, amesema anazingatia pia mahitaji yake katika kipindi cha kunyonyesha.

Aidha, Zuchu ameeleza kuwa maisha yake ya nyumbani yanatofautiana na yale ya nje, akisema akiwa nyumbani ni mama, lakini anapotoka nje hurudi katika nafasi yake ya msanii, jambo linalomfanya aone umuhimu wa kuutunza muonekano wake.

Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu mabadiliko ya mwili baada ya kujifungua na namna akina mama wanavyoweza kusawazisha majukumu ya malezi na mahitaji yao binafsi.

Related Articles

Back to top button