EPLKwingineko
Dabi ya Manchester ni kisasi, patashika

MICHEZO sita ya Ligi Kuu England(EPL) inapigwa leo kwenye viwanja tofauti huku mashabiki wa soka wakisubiri kwa hamu dabi kati ya Manchester United na Manchester City.
Dabi hiyo itapigwa uwanja wa Old Trafford huku Manchester United ikitaka kulipiza kisasi cha kipigo cha mabao 6-3 katika mchezo wa kwanza Oktoba 2, 2022 kwenye dimba la Etihad.
Mechi hiyo inapigwa wakati Kocha wa United Erik Ten Hag amebadili mwenendo wa kikosi hicho katika wiki za hivi karibuni na kuwa bora.
Michezo mingine ya EPL leo ni kama ifuatavyo:
Brighton & Hove Albion vs Liverpool
Everton vs Southampton
Nottingham Forest vs Leicester City
Wolverhamton Wanderers vs West Ham United
Brentford vs AFC Bournemouth