Kuogelea waondoka leo kuelekea Uganda

DAR ES SALAAM: TIMU ya Taifa ya kuogelea imeondoka leo kuelekea Kampala, Uganda, kushiriki Mashindano ya Kuogelea ya Afrika, Kanda ya Tatu, yatakayofanyika kuanzia Oktoba 20 hadi 25 mwaka huu.
Kikosi hicho kina jumla ya washiriki 34 kwa mujibu wa orodha iliyotolewa, kikitarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo yanayokutanisha waogeleaji kutoka mataifa mbalimbali ya ukanda huo.
Miongoni mwa waogeleaji wanaounda kikosi hicho ni Zac Okumu, Isaac Mukani, Alberto Itatiro, Filbertha Demello, Fidel Kavishe, Nicolene Viljoen, Celine Matembo, Abbas Abdulali, Oscar Liebchen na Nabil Ahmed.
Wengine ni Shuneal Bharwani, Ibrahim Igoro, Camilla Kyenekiki, Nolan Maginga, Ethan Makala, Ithra Kahemele, Arthur Mushi, Luke Okore, Austin Okore, Julius Missokia, Max Missokia na Abigail Matungwa.
Waogeleaji wengine ni Mikhail Mangush, Mark Tibazarwa, Cathleen Maokola, Ruby Stanley, Kabeer Lakhani, Leyna Borega, Lorita Borega, Konhelli Mhela, Iris Mattaka na Imaan Kimario.
Mashindano hayo ni sehemu ya jukwaa la ushindani kwa waogeleaji wa Tanzania kupima uwezo wao dhidi ya washiriki kutoka nchi nyingine, huku yakitoa nafasi ya kuimarisha uzoefu wa kimataifa.
Tanzania inaingia katika mashindano hayo ikiwa na jukumu la kuwakilisha nchi kwa ushindani na kutumia fursa hiyo kuendeleza kiwango cha mchezo wa kuogelea.




