Kikapu

The Reel Dream yaikaribia taji la WBDL

DAR ES SALAAM: TIMU ya The Reel Dream iko katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Kikapu ya Wanawake Dar es Salaam (WBDL) 2026 baada ya kuichapa Tausi Royals vikapu 69-44 katika mchezo wa pili wa fainali na kufikisha ushindi wa michezo miwili bila kupoteza.

Matokeo hayo yanaifanya The Reel Dream kusalia na ushindi mmoja pekee ili kutwaa ubingwa wa msimu huu, baada ya kuendeleza ubora wake katika michezo miwili ya mwanzo ya fainali hizo.

Timu hizo zinachuana katika mfumo wa ‘Best of Five’, unaohitaji timu kupata ushindi katika michezo mitatu ili kutawazwa bingwa wa WBDL 2026.

Hata hivyo, macho na matarajio ya timu hizo sasa yanaelekezwa katika mchezo wa tatu unaochezwa leo, ambao unaweza kuamua hatma ya ubingwa endapo The Reel Dream itapata ushindi na kufikisha michezo mitatu ya ushindi.

Kwa upande wa Tausi Royals, mchezo huo ni muhimu katika juhudi za kurejesha ushindani na kuzuia wapinzani wao kutwaa taji, huku ikihitaji ushindi ili kuendeleza matumaini yake ya kubeba ubingwa wa msimu huu.

Related Articles

Back to top button