Deschamps kuinoa Ufaransa hadi 2026
KOCHA Didier Deschamps amekubali kuongeza mkataba kukinoa kikosi cha Ufaransa ‘Les Bleus” hadi mwisho wa michuano ya fainali za Kombe la Dunia 2026.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Ufaransa(FFF) limethibitisha mkataba huo mpya wa Deschamps utaishia Juni 2026.
Hatua hiyo imemaliza hofu iliyokuwepo kwamba angeondoka baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Dunia 2022 Qatar dhidi ya Argentina.
Kwa nyongeza hiyo ya mkataba Deschamps ataiongoza Les Bleus kwenye michezo mwili muhimu ijayo ya kufuzu fainali za Euro 2024 dhidi ya Uholanzi na Ireland michuano itakayofanyika Ujerumani.
‘Ni kitu muhimu katika ufanisi wa timu ya Ufaransa. Nilitambua tangu kurejea kwangu hisia na shauku ambayo Kombe hili la Dunia limeweza kuzalisha,” amesema Deschamps.
Kumekuwa na uvumi kwamba nguli wa Ufarnsa na kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidan angeweza kuchukua mikoba baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia 2022.
Fainali za Kombe la Dunia 2026 zimepangwa kuandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.




