Mastaa

Ray Kigosi na Chuchu Hans watarajia mtoto wa Pili

DAR ES SALAAM:MSANII na muigizaji maarufu nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’, amefichua furaha yake baada ya mpenzi wake, Chuchu Hans, kuwa katika kipindi cha ujauzito wa mtoto wao wa pili.

Ray ameshiriki picha za kifamilia kupitia mitandao ya kijamii, akiambatanisha na ujumbe wa upendo huku akimshukuru Mungu kwa zawadi hiyo kubwa ya kuongeza mtoto katika familia yao.

Katika ujumbe huo, Ray ameeleza kuwa anafurahia kwa dhati hatua hiyo na namna anavyoendelea kujenga familia yake pamoja na Chuchu Hans, ambaye tayari wamejaaliwa mtoto wa kiume, Jaden.

 

“My lovely Mzungu, maneno hayatoshi kueleza furaha na shukrani nilizonazo moyoni. Unakaribia kunipa zawadi ya thamani kuliko zote, mtoto wetu wa pili,” ameandika Ray.

Aidha, Ray amemshukuru Mungu kwa ajili ya Chuchu Hans na baraka hiyo mpya, akieleza kuwa upendo na furaha anayopata katika familia yake ni sehemu muhimu ya maisha yake.

Ameahidi kuendelea kuthamini familia yao, kumpenda Chuchu Hans na kusimama naye katika kila hatua ya maisha yao.

“Nakupenda sana My Lovely Mzungu. Mungu ailinde familia yetu na aibariki familia yetu daima. Nakuahidi kuthamini familia yetu, kukupenda sana na kusimama na wewe katika kila hatua ya maisha yetu,” ameongeza.

Ujauzito huo unatarajiwa kuongeza furaha nyingine katika familia ya Ray na Chuchu, huku mashabiki na watu mbalimbali wakitoa pongezi kwa familia hiyo kwa baraka hiyo mpya.

Related Articles

Back to top button