EPLKwingineko

Gakpo njia nyeupe Liverpool

KLABU ya Liverpool imefikia makubaliano kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Cody Gakpo, klabu ya Philips Sport Vereniging-PSV Eindhoven imetangaza.

Gakpo mwenye umri wa miaka 23 atajiunga na Liverpool kwa pauni zinazoripotiwa kuwa milioni 37 sawa na shilingi bilioni 103.5 baada ya miezi kadhaa ya uvumi ukimhusisha kuhamia Manchested United.

Dili hilo linaweza kupanda hadi puni milioni 50 sawa na shilingi bilioni 139.9 katika nyongeza ya rekodi ya mauzo kwa klabu ya PSV.

“PSV na Liverpool zimefikia makubaliano ya usahamisho ujao wa Cody Gakpo,” imesema PSV kupitia tovuti yake.

Usajili wa Gakpo utasaidia kuboresha safu ya ushambuliaji ya Liverpool wakati Luis Diaz na Diego Jota wakiwa majeruhi.

Gapko amechangia mabao 30 katika michezo 24 ya PSV msimu huu akifunga mara 13 na kutengeneza mmabao 17.

Related Articles

Back to top button