Ni Dabi ya kisasi wanawake leo

LIGI Kuu ya soka ya wanawake Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili huku mechi kivutio ikiwa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga.
Mchezo huo wa raundi ya 3 utapigwa uwanja wa Bejamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa mwisho wa kirafiki timu hizo kukutana Oktoba 22, 2022 Simba Queens iliifunga Yanga Princess mabao 2-0 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mechi hiyo itaamuliwa na mwamuzi wa kati Tatu Malogo kutoka Tanga, mwamuzi msaidizi namba 1 Sikudhani Mkurungwa kutoka Njembe na mwamuzi msaidizi namba 2 Maria Mwakitalima kutoka Mbeya.
Nazo Ceasiaa Queens na Amani Queens zitaoneshana kazi kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Matokeo ya michezo mingine ya raundi ya 3 iliyochezwa Disemba 21 ni kama ifuatavyo:
JKT Queens 3-0 Baobab Queens
The Tigers Queens 1-4 Alliance Girls
Fountain Gate Princess 2-0 Mkwawa Queens