Nyumbani

Coastal yamtimua Chipo

KLABU ya Coastal Union imetangaza kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo Yusuf Chipo.

Taarifa ya klabu hiyo imesema kwa kipindi hiki ambacho timu haitakuwa na kocha mkuu kuanzia mchezo wa leo dhidi ya dhidi Yanga kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Msaidizi Joseph Lazaro.

“Klabu yetu ya Coastal Union inautaarifu umma kuwa imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu Yusuf Chipo kuanzia jana Disemba 19, 2022.” imesema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mchakato wa kutafuta kocha mpya unaendelea.

Chipo alijiunga na Coastal Union kwa mkataba wa mwaka mmoja Septemba 2022 akichukua nafasi ya Juma Magunda aliyeteuliwa na Simba kuwa Kocha Mkuu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button