Filamu

Filamu ya Sinners yashinda tuzo 3 Hollywood

CALIFORNIA: FILAMU ya Sinners imeshinda tuzo tatu kubwa katika tuzo za 16 za Hollywood Music in Media Awards (HMMAs), zilizofanyika Jana Jumatano November 19 katika ukumbi wa The Avalon, Hollywood, California nchini Marekani.

Filamu hiyo imepokea tuzo hizo ikiweka rekodi ya kuwa filamu iliyoshinda tuzo nyingi zaidia ya filamu zote zilizoshindanishwa katika tuzo hizo.

Mtunzi na mtayarishaji maarufu wa filamu hiyo Ludwig Göransson naye ameshinda tuzo kupitia filamu hiyo ya Sinners.

Filamu hiyo iliyoongozwa na Ryan Coogler, kwa sasa ni ya tano kwa makusanyo makubwa kwa mwaka huu ndani ya Marekani.

Watazamaji wengi wameitabiria filamu ya sinners kuingia katika kinyang’anyoro cha tuzo za Oscars 2025 katika vipengele vya muziki.

Jeff Beal mshindi wa Emmy mara tano na msanii wa Afghanistan Aryana Sayeed, walipata nafasi ya kutumbuiza katika tuzo hizo wakiimba wimbo wao wa “We Believe in Hope,” kabla ya Beal kushinda Score Independent Film kwa Rule Breakers.

Related Articles

Back to top button