Nyumbani

Yakoub Suleman atuma ujumbe wa faraja kwa Camara

DAR ES SALAAM: GOLIKIPA wa Simba SC, Yakoub Suleman, ametuma salamu za faraja na pole kwa mlinda mlango mwenzake, Moussa Camara, ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti nchini Morocco.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu ya Simba, Moussa Camara amefanyiwa upasuaji na umekamilika kwa mafanikio nchini Morocco.

Baada ya taarifa hiyo, Yakoub kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii, ameonesha kuguswa na hali ya Camara na kumwandikia ujumbe wa faraja akisema: “Pona haraka kaka. Mungu akufanyie wepesi urudi kwenye afya njema. Kazi na utu.”

Camara alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United na upasuaji wake umekamilika kwa mafanikio.

Anatarajiwa kuanza hatua za awali za ukarabati kabla ya kurejea uwanjani baada ya wiki 8–10 kutegemea na hali yake.

Simba SC itamkosa Camara kwenye mechi za awali za hatua ya makundi lakini nafasi yake kwa sasa itabebwa na Yakoub Suleman.

Related Articles

Back to top button