Muziki

Nitafanya kazi hadi nikiwa na miaka 82

NEW YORK: MWANZILISHI maarufu wa familia ya Kardashians, Kris Jenner, ameshiriki malengo yake mapya baada ya kuadhimisha miaka 70.

Nyota huyo na watoto wake Kim, Kourtney, Khloe, Rob Kardashian, Kendall na Kylie Jenner, amesema anatarajia kuendelea kufanya kazi kwa miaka mingi ijayo kwa kuwa anajilinda kiafya pamoja na kuwa na uhusiano imara na watu waliomzunguka.

Akizungumza na E! News kuhusu malengo yake baada ya kufikisha umri wa miaka 70, Kris alisema, “Mama yangu ana miaka 91 na daima ananieleza kuwa alifanya kazi hadi akiwa na miaka 82. Hii ndiyo ilimsaidia kuwa na uhai na kujisikia kuwa bado ni sehemu ya maisha yake.”

Kris alisherehekea siku yake muhimu kwa sherehe iliyojaa nyota maarufu, akiwemo Beyoncé, Jay-Z, Prince Harry na mkewe Meghan Markle. Kulingana na Us Weekly, sherehe hiyo dada zake wote walikuwa wakiburudika kwa kuimba na kucheza.

Sherehe hiyo ilifanyika nyumbani kwa Jeff Bezos na Lauren Sanchez, na ilikuwa na mada ya James Bond. Hata hivyo, washiriki hawakuwa na ruhusa ya kutumia simu zao ili kuhifadhi kumbukumbu za usiku huo.

Kris ana wajukuu 13, na anataka wawe na furaha wakati wa kipindi hiki cha Krismasi. Alisema, “Wanafurahi sana kwa sababu Santa ana kuja, pamoja na masalie. Wanalala usingizi, sisi tunaenda kuwachukua na kuwafanya wasome The Night Before Christmas. Na asubuhi ya Krismasi, tunakuwa na wakati wa kupendeza sana kama familia.”

Related Articles

Back to top button