Muziki

Rema ataka kufananishwa na Wizkid, Davido na Burna Boy

LAGOS: MWIMBAJI maarufu wa Nigeria Divine Ikubor maarufu Rema, amesema ni dharau kumtofautisha kimuziki na wasanii wenzake wenye majina makubwa nchini Nigeria Wizkid, Davido na Burna Boy.

Mwimbaji huyo amesema hayo alipokuwa akizungumzia sintofahamu kutokana na ujumbe wake wa X alioandika “Hakuna tena ‘Big 3’ kuna ‘Big 4’” ujumbe huo ameutoa katika wimbo wake mpya wa ‘Hehehe,’ aliouachia mapema wiki hii.

Burna Boy, Wizkid na Davido wanajulikana sana kama wasanii wakubwa wa Nigeria na duniani kwa pamoja wanajulikana kama “Big 3” lakini Rema amekuwa akisisitiza kuwa sasa yuko kwenye orodha ya nyota hao na wanatakiwa kuwa “Big 4.”

“Ni matusi kusema siko kwenye kiwango sawa na Wizkid, Davido ama Burna Boy wanaitwa ‘Big 3’ nami nimeongezeka sasa wanatakiwa kuitwa ‘Big 4′ maana ninanguvu kama wao kimuziki na uwezo wa muziki wangu ndani ya Nigeria nan je ya Nigeria una nguvu,” alisema Rema.

Related Articles

Back to top button