Kwingineko

Euro 2028 kutotumia mifumo ya tiketi ya FIFA

LONDON: WAANDAAJI wa Michuano ya Ulaya ya 2028 (Euro 2028) wamesema hawatatumia mfumo wa bei shirikishi za tiketi (dynamic ticket pricing), ambao bei hubadilika kulingana na mahitaji ya mashabiki kwa mchezo husika.

Mfumo huo tata ulitumika kwenye Kombe la Dunia la Klabu lililofanyika Marekani Katikati ya mwaka huu, ambapo bei za tiketi ziliongezeka na kushuka kwa viwango visivyotabirika. FIFA imethibitisha pia kuwa mfumo huo utatumika kwenye Kombe la Dunia la wanaume mwaka ujao, ambapo tiketi zitagharimu kati ya dola 60 kwa mechi za makundi hadi dola 6,730 kwa fainali.

Hata hivyo, waandaaji wa Euro 2028, itakayofanyika England na Ireland, wamesema hawatautumia mfumo huo wa FIFA katika kupanga bei za michuano hiyo itakayotimua vumbi mwaka 2028.

“Hakutakuwa na mfumo wa dynamic ticket pricing. Hilo limekubaliwa wazi. Kuna mambo ya msingi: kwanza, hakuna bei zinazoendeshwa na mahitaji; na pili, takribani nusu ya tiketi zitakuwa katika Kundi la Tatu (Category Three) na pia Fan First, ambalo ni kundi la chini zaidi.” – amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Soka cha England (FA), Mark Bullingham.

Katika michuano ya Euro iliyopita, tiketi za Category Three ziligharimu euro 60 (takriban Shilingi za Tanzania 169,740), huku tiketi za Fan First zikiwa euro 30 (takriban Shilingi za Tanzania 84,870)

Wakati wa Kombe la Dunia la Klabu, mfumo huo wa bei ulisababisha tiketi ya kawaida ya nusu fainali kati ya Chelsea na Fluminense mjini New Jersey kushuka kutoka dola 473.90 (takriban Shilingi za Tanzania 1,196,147.50) hadi dola 13.40 (takriban Shilingi za Tanzania 33,835) jambo lililozua malalamiko ya mashabiki na wadau wa soka walionunua tiketi hizo mapema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button