BurudaniFilamu

BLOODSHOT: Ni vita ya kisayansi kwenye zama za sayansi

NILIPOTAZAMA trela ya Bloodshot kwa mara ya kwanza, nilijikuta navutiwa sana. Na nilipogundua kuwa fi lamu hii iliyotoka Februari 20, 2020 imetokana na kitabu cha michoro ya hadithi (comic book) nikafurahia zaidi.

Unapoanza tu kuitazama sinema hii utaona kwamba unatazama bonge la filamu lililojaa aksheni na hasa kama Vin Diesel ndiye mhusika mkuu. Bahati mbaya, kwenye tukio lolote lisilo la aksheni, Bloodshot inaonekana kuchusha zaidi. Mtazamaji anaweza kubashiri
kinachokwenda kutokea baadaye.

Ndani ya dakika kumi tu nimeweza kugundua kwa usahihi mambo kadhaa makubwa yaliyokuwa hayajatokea. Hali hii imenifanya nishindwe kuvutiwa kabisa na filamu hii. Nimejikuta nashindwa kuzingatia mtiririko wa storinkwa sababu nimeshajuannkitakachotokea mbeleni.

Matukio yenyewe ninmazuri sana, hasa kamanwewe ni shabiki wa filamunza aksheni kama mimi. Lakini matukio yenyenaksheni pekee hayawezi kufanya filamu kuwa nzuri, hasa kutokana na msuko wa stori yenyewe.

Matukio yanaonesha kujirudia haraka sana. Kimsingi, Vin Diesel anafanya jambo lilelile mara zote, kiasi kwamba linachosha. Filamu ya Bloodshot inaonekana kufanana na filamu kama Total Recall au Robocop, ingawa haifanani sana lakini inakaribiana sana na kazi hizo.

Hii ni moja ya sababu inayoweza kukufanya kubashiri kitakachotokea mbeleni. Lakini kama haujawahi kutazama au kusikia kuhusu Total Recall, utaifurahia sana Bloodshot kuliko ilivyonitokea.

Lakini Total Recall ni bonge la filamu la aina yake. Bahati mbaya, hii ndiyo sababu filamu ya Bloodshot haijanivutia. Hata hivyo, jambo zuri kuhusu filamu ya Bloodshot ni kwamba imenipa mshawasha wa kutafuta kitabu cha michoro ya hadithi kwa sababu ninahisi kuwa kinaweza kuwa na kitu bomba zaidi ya kile kinachooneshwa kwenye filamu hii.

Bloodshot imetokana na kitabu cha michoro ya hadithi kilichouza zaidi, ambapo Vin Diesel
anacheza nafasi ya Ray Garrison, askari aliyeuawa na baadaye anarudishiwa uhai na shirika la Rising Spirit Tech (RST) na kuwa shujaa wa Bloodshot.

Mchezo unaanza wakati Ray Garrison na mkewe Gina wanasafiri kwa likizo ya mapumziko
katika mji wa pwani wa Amalfi nchini Italia, baada ya kumaliza misheni ya oparesheni ukombozi jijini Mombasa.

Wakiwa nchini Italia, Garrison na Gina wanatekwa na kikundi cha mamluki kinachoongozwa na Martin Ax, ambaye anadai kujua chanzo cha oparesheni ya Mombasa.

Mamluki hawa wanahitaji maelezo ya kijasusi kuhusu oparesheni hiyo, kwa kuwa Garrison hana analolijua kuhusu habari hii, ukweli wanaoujua wao ni kuwa Garrison hastahili kabisa kuishi.

Ax anamuua kwa risasi moja tu yenye nguvu yeye na mkewe Gina. Ndipo anapoibuka
Dk Emil Harting, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la RST na mwanasayansi wa zama hizi aliyegundua teknolojia ya kumrudishia mtu uhai na kumfanya asiwe binadamu wa
kawaida.

RST wanatumia teknolojia ya special nanite system kwenye mwili wa Garrison na kufanikiwa. Hii ni teknolojia ambayo itaanza kufanya kazi miaka mingi ijayo. Dk Harting haamini kuhusu mafanikio ya ugunduzi wake.

Hata anapokuja kutambua kuwa amefanikiwa, anafanya jaribio jingine la kisayansi linalokuja kuzua kizaazaa.

Anapanga kubadilisha akili za Garrison kutoka alichokuwa anakijua kwenye maisha yake yaliyopita kuja maisha mapya lakini anasahau kuwa Garrison alipoteza mkewe na aliahidi kuwatafuta wabaya wake na kulipa kisasi.

Jaribio la kisayansi la kumfanya Garrison asiwe na kumbukumbu ya kilichotokea nyuma linabadilika kuwa la kumfanya Garrison awe nusu mtu nusu mashine. Ni hapo ulimwengu unapochafuka.

Kutaka kumrudisha Garrison maabara ni kama kumtafuta mtoa roho kwa tochi. Hashikiki wala haambiliki!

Anawataka watu wake! Wakati Dk Harting akitafuta suluhisho la Garrison anaamini kwenye maabara yake yupo Eric, mtaalamu wa udukuzi wa kompyuta ambaye ana uwezo wa kuufanya ubongo wa binadamu ucheze muziki anaoutaka.

Jambo analosahau ni kwamba kila fundi ana fundi wake. Ndiyo… wakati Garrison
akitafuta msaada wa kuondoka kwenye mikono ya Dk Harting ili asiondolewe uwezo wake wa kumbukumbu, anakutana na Wilfred Wigan, Mmarekani mwenye asili ya Afrika ingawa Garrison haamini kama atamsaidia.

Hapa kuna funzo kubwa; tusiwadharau watu kwa mwonekano wao! Garrison akiamini
Wigan hana analolijua ndipo anapogundua kuwa vidole vya Wigan ndivyo vilivyomfundisha Eric wa maabara ya Dk Harting jinsi ya kuitumikisha special nanite technology system.

Hata Dk Hart anapomuuliza  Eric ni nani kaingilia mfumo wa nanite technology anapata jibu kuwa ni “mwalimu wangu”, na sasa hakuna tena jinsi ya kumzuia Garrison huko mtaani, maana yupo kwenye mikono ya mtu anayeujua mfumo mzima hadi mfumo wenyewe
unamwogopa.

Dk Harting anaingia mstari wa mbele kupambana na Garrison lakini hajui Garrison si binadamu tena bali ‘nanite system’ iliyokamilika. Hapo ndipo inakuwa vita ya kisayansi
kwenye zama za sayansi.

Related Articles

Back to top button