World Cup

Saudi Arabia yaiduwaza Argentina

Miamba ya soka duniani Argentina imepokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Saudi Arabia katika mchezo wa kundi C michauno ya Kombe la Dunia inayoendelea Qatar.

Argentina ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia nahodha wake Lionel Messi kwa njia ya penalti katika dakika 10 wakati wa mchezo uliofanyika uwanja wa Lusail.

Baada ya mapumziko Saudi Arabia ilianza juhudi za kusawazisha na kufanikiwa kupata bao dakika 49 likifungwa na Saleh Al-Shehri.

Bao la ushindi la Saudi Arabia lilipatikana dakika ya 53 ya mchezo likifungwa na Salem Al-Dawsari.

Baada ya bao hilo la Saudi Arabia, Argentina ilijaribu kusawazisha lakini bila mafanikio hadi mwisho wa mchezo.

Michezo mingine miwili inafanyika baadaye leo kundi D ambapo Denmark itavaana na Tunisia huku Ufaransa ikipepetena na Australia.

 

Related Articles

Back to top button