Featured
TFF, UNFPA kushirikiana kijamii
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) yamesaini makubaliano ya ushirikiano katika kampeni za mambo mbalimbali ya kijamii.
Rais wa TFF, Wallace Karia na Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA, Mark Bryan Schreiner wamesaini makubaliano ya ushirikiano huo leo Dar es Salaam.
UNFPA ni shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia afya ya uzazi na jinsia.




