Kwingineko

“Lengo letu ni kutwaa kombe la Dunia” – Nagelsmann

BRATISLAVA: KOCHA Julian Nagelsmann wa Mabingwa mara nne wa dunia Ujerumani ameweka wazi malengo yao ya dhati ya kutwaa Kombe la Dunia la 2026 mbele ya waandishi wa Habari katika mkutano wa kabla ya mechi yao ya kwanza ya kufuzu dhidi ya Slovakia leo Alhamisi.

Ujerumani itaanza kampeni ya Kundi A kufuzu Kombe la Dunia ugenini mjini Bratislava saa 3:45 usiku wa leo kabla ya kuwakaribisha Ireland Kaskazini Septemba 7 mjini Cologne.

Nagelsmann amesema wana hamu ya kuanza kwa ushindi katika harakati zao za kufuzu kwa michuano hiyo itakayoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico mwaka ujao.

“Ni vyema kuweka malengo. Ni vigumu kwa timu au hata mtu binafsi kutoboa maisha bila lengo analofanyia kazi, ambalo ni muhimu kupigania,” Nagelsmann aliuambia mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa ikiwa ana lengo la kushinda Kombe la Dunia”.

“Nafikiri ni vyema kwamba sote tunataka kushinda Kombe la Dunia. Nina hakika 100% kwamba hakuna mchezaji ambaye ana majibu tofauti au hatahitaji kusafiri nasi kufikia lengo hilo” – Nagelsmann alisema.

“Lakini tunahitaji kupitia mchakato sahihi hadi tufike huko, kwa kila mchezo, Ili kutokuwa na wakati wa shaka kwa sababu ya kuweka lengo kubwa. Mchakato ni muhimu kufikia malengo.” aliongeza

Ujerumani, ambayo ilitolewa katika robo-fainali ya michuano ya Euro 2024 kibarua cha kwanza kwa Nagelsmann, imepoteza mechi zao mbili za mwisho mwezi Juni kwa kufungwa na Ureno na Ufaransa kwenye UEFA Nations League.

Ujerumani pia ilitolewa katika hatua ya makundi katika matoleo mawili ya mwisho ya Kombe la Dunia na kura za maoni za ndani ya taifa hilo zimeonesha si mashabiki wote wanaoamini kama wataweza kuvuka chini ya kocha Nagelsmann.

Related Articles

Back to top button