Burudani

Jux amuandalia sherehe ‘mfululu’ Rakeem

DAR ES SALAAM: MSANII maarufu wa Bongo Fleva, Juma Mkambala maarufu kama Jux, amesema mashabiki wake waendelee kumfuatilia kwa karibu kwani anaandaa sherehe nyingi zaidi kufuatia ujio wa mtoto wake wa kwanza Rakeem.

Jux amesema kuwa mtoto wake Rakeem ni baraka kubwa, na kama baba mpya, ana kila sababu ya kusherehekea kwa kiwango kikubwa

“Huyu ni mtoto wangu wa kwanza, lazima nifanye sherehe nyingi. Zina faida hata kwa nchi yetu kwa sababu ninaleta wageni wengi kutoka nje ya nchi,” amesema Jux.

Msanii huyo amekumbusha namna harusi yake iliyofanyika JP ilivyoingiza zaidi ya wageni 200 waliotembelea Tanzania, akisisitiza kuwa tukio la sasa litakuwa kubwa zaidi.

Related Articles

Back to top button