Muziki
Ali Kiba na Khadija Kopa waachia ‘kombora’

DAR ES SALAAM: MSANII nguli wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’,ameshirikiana na Malkia wa taarab Khadija Omary Kopa kutoa wimbo mpya wa kisiasa uitwao “Wameshachelewa”, ukiwa ni wimbo maalumu wa kuunga mkono marais Samia Suluhu Hassan na Hussein Ali Mwinyi kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Wimbo huo wenye ladha ya taarab umebeba ujumbe mzito kwa wapinzani, wakisema wazi kuwa “wameshachelewa” kuleta mbadala wa viongozi hao wawili, kwa kuwa wananchi tayari wameona mafanikio ya utawala wao.
Kupitia mtandao wa Instagram, Kiba na Khadija Kopa wameutambulisha rasmi wimbo huo pamoja na video yake