Ligi KuuNyumbani

Simba kurudisha makali leo?

BAADA ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Singida Big Stars katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Simba leo inashuka dimbani kuikabili Ihefu.

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 9 wakati Ihefu inashika mkia nafasi ya 16 ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 9.

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu leo Azam ni wageni wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu uliopo Turiani, Morogoro.

Azam ipo nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 20 baada ya michezo 10 wakati Mtibwa Sugar inashika nafasi 7 ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 10.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button