EPL

EPL kuja na mabadiliko haya Matano

LONDON: Ligi kuu ya England inatarajia kufungua pazia lake leo Agosti 15 kwa mtanange mkali baina ya mabingwa watetezi Liverpool dhidi ya AFC Bournemouth katika dimba la Anfield huku kukiwa na mabadiliko makubwa Matano katika kanuni za Ligi hiyo. Spotileo inakusogezea mabadiliko hayo Matano kwenye EPL

Kwanza marekebisho ya kanuni ya kupoteza muda (Time wasting rule), kanuni hii sasa inatoa adhabu ya pigo la Kona kwa timu pinzani ikiwa golikipa wa timu inayoanzisha mashambulizi atakaa na mpira bila kuurudisha mchezoni kwa sekunde nane.

Pili kutakuwa na mahojiano baina ya wanahabari au kituo cha Televisheni chenye haki ya matangazo ya ligi hiyo kabla ya mechi kumalizika kwenye ‘Touchline’ na hii itahusisha pia mchezaji ambaye amefanyiwa mabadiliko punde.

Tatu Ili kupunguza mizozo ya uwanjani, manahodha wa timu pekee ndio wanaoruhusiwa kuwasiliana na waamuzi wakati wa mechi. Ikiwa nahodha ni golikipa, mchezaji aliye bench anaweza kuchukua jukumu hilo na kuwa mpatanishi. Wachezaji watakaokiuka kanuni hii wanaweza kuonywa kwa kadi ya njano.

Tatu hatua kali zaidi za penalty, Waamuzi sasa wanaweza kutoa penalti kwa mchezaji kutumia mikono yote miwili kumzuia mpinzani aliye ndani ya box wakati mpira wa adhabu ‘foul’ utakapokuwa ukipigwa kuelekea langoni na hii ni baada ya kutoa onyo moja pekee. Mabadiliko haya yanalenga kutunza mud ana kuondoa mizozo na kusukumana wakati mpira ukiwa unaelekezwa golini.

Nne mchezaji ataruhusiwa kurudia kupiga penalty ikiwa aliugusa mpira mara mbili bila kukusudia na ikiwa atafanikiwa kufunga, hapa inamaanisha labda mpira umegusa mguu wake mwingine kabla ya kupiga penalty yenyewe ikiwa atakosa timu inayolinda itapata ‘indirect free kick’

Tano teknolojia, Ligi kuu ya England sasa itatumia teknolojia zaidi katika kuongeza msisimko zaidi. Waamuzi sasa watavaa camera za mwili (Ref-Cams) katika baadhi ya mechi kama ilivyoonekana katika mechi za Kombe la Dunia la Klabu lililomalizika hivi karibuni. Maamuzi ya VAR sasa yatatangazwa kwa mashabiki viwanjani huku pia Premier League ikitambulisha kampuni ya Puma kama msambazaji mpya wa Mpira rasmi wa mechi na kusitisha miaka 25 ya Adidas katika Nyanja hiyo.

Related Articles

Back to top button