Inaki na Nico kucheza timu tofauti Kombe la Dunia
Wachezaji wawili ndugu Inaki na Nico Williams wanaelekea fainali za Kombe la Dunia huko Qatar mwezi huu wakicheza timu tofauti za taifa.
Inaki atawakilisha taifa la wazazi wake Ghana wakati Nico atakuwa sehemu ya kikosi cha Hispania.
Washambuliaji hao wawili wameisaidia Klabu ya Athletic Bilbao kuanza vyema msimu wa La Liga ambayo ipo nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi.
Inaki will be representing Ghana after finally accepting their offer to switch nationalities from the country of his birth to that of his parents. He made his debut for the Black Stars in September against Nicaragua and also played against Brazil.
Inaki ataiwakilisha Ghana baada ya hatimaye kukubali kubadili uraia kutoka wa kuzaliwa kwenda uraia wa wazazi wake.
Alianza kucheza timu ya taifa ya Ghana ‘Black Satars’ Septemba 2022 dhidi ya Nicaragua na pia dhidi ya Brazil.
Nico anajiandaa kwenda Qatar akiwa na kikosi cha Hispania akiwa ameitwa kwa mara ya kwanza Septemba katika michuano ya Ligi ya Mataifa UEFA.
Alianza kucheza timu hiyo ya taifa Hispania katika mechi dhidi ya Uswisi na mechi ya pili akitokea benchi dhidi ya Ureno akitoa pasi ya bao la ushindi la Alvaro Morata lililoiwezesha Hispania kutinga nusu fainali.



