Chelsea wako ‘siriazi’ na Xavi Simons

LEIPZIG: inaelezwa kuwa mabingwa wa Dunia Chelsea wamewafahamisha RB Leipzig nia yao ya dhati kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Uholanzi Xavi Simons ambaye Klabu yake hiyo ya Bundesliga iko tayari kumuuza mchezaji huyo msimu huu wa joto.
Kwa mujibu wa mwanahabari za michezo wa kituo cha Sky Sports Ujerumani Florian Plettenberg, mazungumzo kati ya pande hizo yameendelea vizuri. Makubaliano ya mdomo kati ya Simons na Chelsea yamefikiwa, lakini bado hayajakamilika kwani bado kuna baadhi ya maelezo ya kufanyiwa kazi.
Leipzig wameweka dau la chini ya Euro milioni 70 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye anaonekana kuwa mmoja wa wachezaji ya kutumainiwa si tu ndani ya klabu yake bali kwa maendeleo ya soka la kisasa barani Ulaya.
Msimu uliopita Simons alifikisha mabao 13 na asisti 9 katika mechi 39 alizocheza akiwa mmoja wa wachezaji mashuhuri kwenye Ligi kuu ya Ujerumani.
Wakati huo huo Leipzig pia wanafanya kila wawezalo kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea Carney Chukwuemeka mwenye umri wa miaka 21 anayeonekana kama mbadala wa Simons