Nyota wa Hollywood Michael Madsen amefariki dunia

CALIFORNIA: MWILI wa nyota wa Hollywood Michael Madsen, ambaye alikuwa katika filamu kadhaa za Quentin Tarantino ikiwemo ‘Kill Bill’ umepatikana nyumbani kwake huko Malibu, California akiwa amefariki dunia.
Meneja wake alithibitisha kifo chake akidai kimetokana na mstuko wa moyo, na amefariki akiwa na miaka 67 lakini taarifa za awali kuhusu kifo chake zinaelezwa kuwa ni ulevi wa kupitiliza na ugonjwa wa moyo.
Taarifa kutoka kwa wawakilishi wake iliyotolewa baada ya mkasa huo ilisomeka: “Katika miaka miwili iliyopita Michael Madsen amekuwa akifanya kazi nyingi kubwa na filamu huru ikiwa ni pamoja na filamu zinazokuja za ‘Resurrection Road’, ‘Concessions na Cookbook za Southern Housewives’, na alikuwa akitarajia kwa hamu kuendelea na kazi hiyo hivi karibuni.
“Madsen pia alikuwa akijiandaa kutoa kitabu kipya kiitwacho ‘Tears For My Father: Outlaw Thoughts and Poems’. Michael Madsen alikuwa mmoja wa waigizaji mashuhuri wa Hollywood, ambaye atakumbukwa na wengi.”
Taaluma ya filamu ya mwigizaji huyo ilidumu kwa miongo kadhaa, kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1980. Mapumziko yake makubwa ya mapema yalikuja 1992 wakati, akiwa na umri wa miaka 35, alishirikiana vyema na muongozaji wa filamu zake katika kazi zake zote ikiwemo ‘Kill Bill: Volume 2’, ‘The Hateful Eight’, na ‘Once Upon a Time’.




