Kwingineko

Kifo cha Jota: Klopp amuandikia barua

LEIPZIG: Meneja wa zamani wa Liverpool Jürgen Klopp ameandika barua kuomboleza kifo cha Diogo Jota mshambuliaji wa Liverpool aliyefariki kwa ajali ya gari ambaye wakati mshambuliaji huyo anatua klabuni hapo Klopp ndie alikuwa kocha wa kikosi hicho.

Katika barua yake Klopp ameandika “Huu ni wakati ambapo ninatatizika sana! Lazima kuna kusudi kubwa zaidi! Lakini siwezi kuliona! Nimeumia, moyo wangu umevunjwa na habari kuhusu kufariki kwa Diogo na mdogo wake André”.

“Diogo hakuwa tu mchezaji mzuri … lakini pia alikuwa rafiki mkubwa, mume na baba mwenye upendo na anayejali! Kila mtu”.

“Tutakukumbuka sana! Maombi yangu yote na mawazo ni kwa Rute (mke wa Jota), watoto, familia, marafiki na kila mtu aliyewapenda. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki”.

“Pumzika kwa amani, Diogo … Tunakupenda”

Barua hii ya Klopp ni miongoni mwa salamu za pole zinazoendelea kumiminika kutoka kwa watu mashuhuri duniani kote, ndani na nje ya tasnia ya michezo. “Wanasema tunapoteza watu tu tunapowasahau, Sitakusahau kamwe” Rúben Neves, rafiki wa karibu wa Jota na mchezaji mwenzake wa zamani wa Wolves ameandika kwenye instagram.

Related Articles

Back to top button