Michezo Mingine

Aurobindo, Alliance, Raah zang’ara

DAR ES SALAAM: MASHINDANO ya Petrofuel TCA Caravan T20 Cup ya Kriketi yameendelea kushika kasi jijini Dar es Salaam, huku timu tatu Aurobindo AKSCV, Alliance Caravans na RAAH Upanga zikiibuka na ushindi wa kishindo katika michezo iliyopigwa kwenye Viwanja vya Gymkhana.

Katika mchezo wa kwanza, Aurobindo AKSCV walionesha ubabe kwa kuichapa Flashnet Aces kwa wicket sita.

Flashnet Aces walitangulia kupiga na kufikisha mikimbio 166 kwa hasara ya wachezaji watano (166/5). Aurobindo walijibu kwa kishindo wakifikisha 167 kwa hasara ya wachezaji wanne (167/4) na hivyo kujihakikishia ushindi huo muhimu.

Mchezo wa pili uliwakutanisha mabingwa watetezi Alliance Caravans na Park Mobile Lions, ambapo Alliance walipiga mikimbio 163/5 kabla ya kuwabana wapinzani wao hadi kufunga 123 wote (123/10).

Kwa matokeo hayo, Alliance walishinda kwa mikwaju 40 na kuendeleza rekodi yao nzuri kwenye michuano hiyo.

Katika mchezo mwingine, RAAH Upanga walitawala mchezo dhidi ya Harab Motors Pak Stars kwa ushindi wa mikwaju 36.

RAAH walipiga mikimbio 184 kwa wachezaji sita (184/6) na kuwazuia Pak Stars kufikia lengo hilo kwa kuwabakiza kwenye 148 kwa wachezaji saba (148/7).

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button