Kaze matumaini ya ushindi ugenini

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema timu hiyo inakwenda Tunisia mapema ili wachezaji wazoee haraka hali ya hewa lengo likiwa kushinda mchezo wa marudiano dhidi ya Club Africain na kutinga hatua ya makundi.
Akizungumza na SpotiLeo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) Dar es Salaam leo klabu ya timu hiyo kuondoka kocha huyo amesema baada ya kuwatambua uwezi wa wapinzani hao katika mchezo wa kwanza anaamini timu yake itapata ushindi ugenini.
“Tumejiandaa vizuri tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini bado nafasi ya kwenda makundi tunayo ndio maana tunakwenda mapema ili wachezaji kuzoea hali ya hewa na kuepuka fitna,” amesema Kaze.
Kocha huyo amesema wameondoka na wachezaji 22 ambao anaamini watafanikisha matokeo mazuri.
Mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji Club Africain na Yanga utafanyika Novemba 9, 2022.