‘ The Walking Dead’ Msimu wa 3 kuoneshwa Septemba 7

PARIS: MSIMU wa 3 wa filamu ya ‘The Walking Dead’ unatarajiwa kuzinduliwa kwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza mnamo Septemba 7, 2025.
Kulingana na ripoti ya Variety. Kipindi cha filamu hiyo kitaoneshwa saa 9 jioni ET/PT kupitia AMC na AMC+.
Mtandao huo umetoa kicheshi kipya na picha za kipekee za muonekano wa kwanza kabla ya uzinduzi.
Filamu hiyo ya mazombi inaendelea kuwaonesha washiriki wakuu Norman Reedusakicheza kama Daryl Dixon na Melissa McBride akicheza kama Carol wakiendelea na safari ya kujiokoa licha ya kupata changamoto kubwa katika sehemu wanazopita.
Norman Reedus kipenzi cha shabiki kutoka franchise mwenye asili ya Walking Dead katika onesho hilo anaoneshwa kushangaza kutokana na kuwasili kwake huko Ufaransa, ambapo anakabiliana na maswali yasiyo na majibu kuhusu jinsi alivyoishi mbali na nyumba kwake.
Safari yake hiyo kutoka Ufaransa inakuwa na misukosuko isiyotarajiwa ambayo inabadilisha mipango yake.
Msimu wa pili, unaoitwa Kitabu cha Carol, ulifanya muhtasari kutoka kwa matukio ya Msimu wa 1. Ambapo Daryl na Carol Peletier, uliochezwa na Melissa McBride, wahusika wote wawili walikuwa wakikabiliana na historia yao.
Wakati Carol alijaribu kumtafuta rafiki yake aliyepotea, Daryl alipambana na matokeo ya kubaki Ufaransa. Mivutano iliongezeka ndani ya Nest, na harakati za Genet zikazidi, zikimsogeza Pouvoir karibu na kufungua mzozo na Muungano wa Matumaini na sasa imekuja Season 3 Je, itataua mzozo huo?