Filamu

Muigizaji India adakwa kesi ya dawa za kulevya

CHENNAI: MUIGIZAJI wa Kitamil-Telugu, Srikanth amekamatwa na polisi huko Chennai leo Jumatatu Juni 23, 2025 baada ya kutajwa katika kesi ya dawa za kulevya.

Kulingana na ripoti ya News18, muigizaji huyo maarufu kwa jina la Sriram alikamatwa baada ya vipimo vya afya kuonesha kuwa anatumia mihadarati na pia miamala ya makosa mbalimbali ya usambazaji wa dawa hizo ilipatikana kwenye simu yake.

Muigizaji huyo alidaiwa kununua kokeini kwa dola12,000 kwa gramu karibu mara 40. Zaidi ya hayo, uchunguzi wa damu ulithibitisha matumizi ya dawa za kulevya, kulingana na ripoti ya vipimo.

Kitengo cha Ujasusi cha Kupambana na Dawa za Kulevya cha polisi wa Chennai (ANIU) kiliripotiwa kumhoji muigizaji huyo, na vipimo vilifanywa katika hospitali ya serikali na polisi walimkamata Srikanth chini ya Sheria ya Dawa za Kulevya na Dawa za Kisaikolojia (NDPS).

Srikanth alipata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 2000 alipoigiza katika filamu mbalimbali za Kitamil na Kitelugu ikiwemo ‘Nanban’, ‘Okariki Okaru’, ‘Oru Naal Oru Kanavu’ na ‘Adavari Matalaku Ardhalu Verule’.

Related Articles

Back to top button