Nyumbani

Msamaha wa kodi vifaa michezo ya kubahatisha

DODOMA: SERIKALI imetangaza kufutwa rasmi kwa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) uliokuwa ukitolewa kwenye ununuaji na uingizaji wa vifaa vya michezo ya kubahatisha (gaming supplies).

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma leo na Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha mapendekezo ya serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/26.

Amesema hatua hiyo inalenga kuleta usawa katika utozaji wa kodi kwa kuwa michezo mingine kama vile mpira wa miguu ipo katika wigo wa utozaji wa kodi ya ongezeko la thamani.

Dk Nchemba amesema hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 322,022.5.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button