Muigizaji Ozark Harris Yulin amefariki

LOS ANGELES: MUIGIZAJI wa filamu ya ‘Scarface’, na tamthilia ya ‘Ghostbusters II’, amefariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo, meneja wake Sue Leibman amethibitisha kifo hicho.
Nyota huyo wa Hollywood amefariki akiwa na miaka 78, ameacha mke Kristen Lowman binti yake Claire Lucido aliyezaa na mke wake wa kwanza Gwen Welles ambaye amefariki dunia mwaka 2021 kufuatia kuugua kwa muda mrefu.
Staa huyo wa filamu mzaliwa wa Los Angeles, Harris amecheza kwa mara ya kwanza katika utayarishaji wa filamu ya James Saunders ‘Next Time I’ll Sing to You’ lakini hakufanikiwa kufika Broadway hadi 1980, alipoigiza katika filamu ya ‘Watch on the Rhine’.
Alikuwa mtu wa kawaida kwenye skrini katika miaka ya 1970 na 1980, na alijulikana kama polisi fisadi akitumia jina la Mel Bernstein katika filamu ya ‘Scarface’ lakini pia alionekana katika sinema maarufu kama ‘Candy Mountain’, ‘Fatal Beauty’ na ‘Another Woman’.