Africa

Twiga Stars mambo yameiva Cecafa

DAR ES SALAM: MCHEZAJI wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’, Fatuma Issa amesema maandalizi yameiva na wako tayari kupambana katika michuano ya wanawake ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inayotarajiwa kuanza kesho.

Michuano hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam na kushirikisha nchi za Uganda, Burundi, Sudan Kusini na Kenya.

Akizungumzia maandalizi yao Dar es Salaam leo, Fatuma, ambaye pia ni nyota wa kikosi cha Simba Queens, amesema mashindano hayo ni fursa ya kipekee kwa wachezaji kuonesha uwezo wao na kujiweka tayari kwa mashindano ya kimataifa.

“Naomba Watanzania na mashabiki wetu waendelee kutusapoti na kutuamini. Tumejiandaa vizuri na tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri,” amesema.

Mashindano hayo sio tu ni muhimu kwao kwa ajili ya kutetea heshima ya taifa, bali pia kama sehemu ya maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2024), zitakazofanyika baadaye mwaka huu.

Twiga Stars itaanza kurusha karata zake dhidi ya Sudan Kusini kesho saa moja usiku. Lakini mchezo wa utangulizi utakuwa ni Uganda dhidi ya Burundi saa 10:00 jioni.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button