Muigizaji aliyefanyiwa upasuaji wa saratani ya ini ametoka ICU

MUMBAI: MUIGIZAJI wa filamu za India, Shoaib Ibrahim ameeleza kwamba mkewe Dipika Kakar ambaye pia ni muigizaji aliyekuwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kwa ajili ya upasuaji wa saratani ya ini kwa sasa ametoka katika chumba hicho na anaendelea vizuri.
Katika video yenye ujumbe kwa mashabiki wao aliyoiweka katika channel yake ya Youtube amesema mkewe Dipika Kakar, amefanyiwa upasuaji wa saratani ya ini ambapo upasuaji huo ulichukua saa 14 kwa kuwa saratani hiyo ilikuwa hatua ya pili.
Video hiyo yenye dakika saba imeeleza kwamba Dipika yuko nje ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na anaendelea kupata nafuu akiwa hospitalini hapo.
Dipika Kakar na Shoaib Ibrahim walifunga pingu za maisha mwaka 2018.
Kabla ya upasuaji huo Shoaib anasema mkewe Dipika Kakar ulikuwa mgumu kuamini kama ungefanikiwa.
Shoaib amefafanua kwamba madaktari walimfanyia upasuaji wa ini mkewe Dipika, na sehemu ndogo ya ini ilikatwa kwa sababu ya uvimbe huo lakini pia mkewe huyo pia alifanyiwa upasuaji wa kibofu cha mkojo.
“Mke wangu Dipika alilazimika kukaa ICU kwa siku tatu. Na atakaa hapa kwa siku tatu hadi tano, kama alivyoshauriwa na madaktari. Upasuaji ulikuwa mkubwa… nawashukuru kwa maombi yenu nyote” amesema Shoaib.