Azam FC yamaliza kazi kwa Aishi Manula

DAR ES SALAAM: KLABU ya Azam FC imetajwa kumrejesha golikipa wake wa zamani Aishi Manula .
Manula anarejea baada ya kuitumikia Simba misimu nane. Msimu huu hakupata nafasi ya kucheza kunako klabu yake hiyo nafasi yake ikichukuliwa na kipa Moussa Camara.
Manula alijiunga na Simba akitokea Azam FC mwaka 2017. Taarifa za chini zinaeleza kuwa ameshamalizana na klabu yake hiyo ya zamani na kwamba anasubiri muda muafaka wa kutangazwa.
Hata hivyo, Msemaji wa Azam FC Thabit Zakaria, ameliambia SpotiLeo kuwa hakuna ukweli wa taarifa hizo, akisisitiza umuhimu wa kusubiri muda ufike ili kujua ukweli zaidi.
Zakaria amesema wakimuhitaji mchezaji yeyote watamsajili na muda ukifika wa kumtangaza watamweka hadharani.
Manula amekuwa akitajwa tangu msimu uliopita kwamba atarajea Chamazi na kupewa nafasi ya kuwa golikipa namba moja baada ya kupoteza matumaini Simba.




