Filamu

Brad Pitt kurudi na filamu ya ‘F1’ Juni 28

NEW YORK: MKALI wa filamu Brad Pitt mwenye miaka 61 anatarajiwa kurejea kwa kishindo na filamu yake ya ‘F1’ inayotarajiwa kutoka Juni 28.

Katika mahojiano na GQ, aPitt amesema: “Nilijiuliza: Je! Nina hadithi zaidi za kusimulia? Je, nina chochote cha kuongeza katika hili? Je, bado kuna msisimko wowote ninaoweza kupata kutokana na hili? Ikaja wazo la ‘F1’ likanipa nguvu zaidi kurudi katika filamu.”

‘F1’ ni tamthilia ya michezo iliyoongozwa na Joseph Kosinski na kutayarishwa na Jerry Bruckheimer, Lewis Hamilton na Brad Pitt.

Katia filamu hii Pitt anacheza kama Sonny Hayes, dereva wa zamani wa Formula One ambaye anarudi kwenye mchezo huo kumshauri kijana, anayechezwa na Damson Idris.

Waigizaji wengine ni pamoja na Kerry Condon, Tobias Menzies, na Javier Bardem.

Utayarishaji wa filamu ya ‘F1’ ulifanyika katika hafla mbalimbali za Grand Prix, ikijumuisha British Grand Prix huko Silverstone, ili kunasa matukio halisi ya mbio za magari.

Utayarishaji huo ulihusisha ushirikiano na timu zote kumi za Formula One na madereva wao, ikilenga kutoa taswira halisi ya mchezo huo.

Onyesho la kwanza la New York City la ‘F1’ limepangwa 16 Juni 2025, likifuatiwa na onyesho la kwanza la London katika Leicester Square mnamo 23 Juni 2025.
Toleo lake linalingana na Austrian Grand Prix ya 2025.

Mbali na ‘F1’, Brad Pitt amefanya filamu nyingine iliyoongozwa na David Ayer huko Queenstown, New Zealand ikimuonyesha Pitt kama mwanajeshi wa zamani wa Jeshi la Wanamaji aliyekwama katika msitu wa Alaska. Filamu hiyo pia imeigizwa na J.K. Simmons na Anna Lambe.

Related Articles

Back to top button